Wavulana Waamua Kuvaa Sketi Shuleni Nchini Uingereza
Takriban wavulana 30 wamevaa minisketi kuenda shuleni wakiandamana kupinga, baada ya kuambiwa kuwa hawaruhusiwi kuvaa kaptula.
Wanafunzi hao walikuwa wameomba ruhusa ya kubadilisha sare zao kutokana na kupanda kwa viwango vya joto.
Mwalimu mkuu wa shule, Aimee Mitchel alisema kuwa kaptula hazikuwa kati ya sare za shule.
Wanafunzi walisema kuwa hatua ya kufanya maandanao ilitokea baada ya mwalimu mkuu ambaye alikuwa ametoa pendekezo hilo la kuvaa sketi awali, licha ya wanafunzi kusema walihisi hakumaanisha kusema hivyo kabisa.
Wanasema wana matumaini kuwa shule itaangalia upya sera za kuvaa katptula kutokana maandamano hayo "Kaptula kwa sasa si sehemu ya sare zetu kwa wavulana na siwezii kufanya mabadiliko yoyote bila ya kuaomba ushauri wa wazazi na familia zao.
"Hata hivyo kutokana na kuwepo majira ya joto, ninatarajia kuwepo mabadiliko siku za usoni," Bi Mitchell alisema.
No comments