Header Ads

Tutahakikisha Ronaldo Hapati Mpira - Chile



Cristiano Ronaldo
Chile itajaribu kuzuia mipira kutomfikia nyota wa timu ya Ureno Cristiano Ronaldo wakati mataifa hayo mawili yatakapokutana katika kipute cha nusu fainali cha kombe la Mabara mjini Kazan kulingana na Kiungo Wa Timu Hiyo Marcelo Diaz.
Mshambuliaji wa Real Madrid Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 alifunga mara mbili kuisaidia nchi yake kufika katika hatua hiyo nchini Urusi.
Sote tunajua kuwa ni mchezaji mzuri, ni hatari sana na anaweza kubadilisha mechi akiwa pekee. Amekuwa na msimu mzuri.Anacheza hapa na nguvu zilezile.
Hatma ya Ronaldo  haijulikani huku kukiwa na ripoti kwamba anataka kuondoka Real Madrid baada ya kushutumiwa kukwepa kulipa ushuru na mamlaka za nchini Hispania.
Lakini yuko katika hali nzuri uwanjani baada ya kufunga mara 16 katika mechi 10 zilizopita kwa klabu na taifa.
''Swala muhimu hapa ni kumzuia kupata mipira'', alisema Diaz.
Mkufunzi wa Ureno Fernando Santos atachunguza hali ya kiungo mpya wa Manchester City Bernado Silva ambaye alihisi uchungu mwingi katika mguu wake wa kulia baada ya kufunga katika mechi ya ushindi siku ya Jumamosi dhidi ya New Zealand

No comments

Powered by Blogger.