Tetesi za Usajili Barani Ulaya Jumatano 21.06.2017
Mabingwa wa England Chelsea wanataka kumsajili
mshambuliaji wa kimataifa wa Poland na Bayern Munich Robert Lewandowski, 28
(Daily Mirror).
Tottenham wanataka pauni milioni 45 kumuuza beki Kyle
Walker, 27, ambaye anasakwa na Manchester City (Daily Star).
Arsenal wamewaambia Barcelona kuwa beki wake Hector
Bellerin, 22, hauzwi na wana uhakika mchezaji huyo wa kimataifa wa Spain
atabakia Emirates (Independent).
Arsenal wanajiandaa kutoa euro milioni 30 kumsajili kiungo
wa Barcelona Arda Turan (Marca).
Arsenal
lazima wasubiri mpaka michuano ya Kombe la Shirikisho la Mabara la Fifa
imalizike ili kufahamu msimamo wa Alexis Sanchez kuhusu mustakbali wake
Emirates (Evening Standard).
Arsenal pia wameanza mazungumzo ya mkataba mpya na kiungo
Aaron Ramsey, 26, ili kuondoa utata wowote kuhusu mustakbali wake (Daily
Telegraph).
Real Madrid wanafikiria kumsajili Alexis Sanchez, ili kuziba
nafasi ya Cristiano Ronaldo (Don Balon).
Juventus nao wanamtazama beki wa Arsenal Hector Bellerin
(Tuttosport).
Juventus pia wanamtaka beki wa Manchester United Matteo
Darmian, 27, kuziba nafasi ya Dani Alves, ambaye anatazamiwa kuondoka Italy
(Goal.com).
Dani Alves, 34, yuko tayari kusaini mkataba wa miaka miwili
na Manchester City, mara atakapokamilisha mazungumzo yake na Juventus (Daily
Mail)
Manchester United itakuwa kimbilio pekee kwa Cristiano
Ronaldo iwapo ataondoka Real Madrid, kwa mujibu wa washauri wake (Daily
Record).
Lakini rais wa Real Madrid Florentino Perez ameelezea sakata
la mustakbali wa Ronaldo kama "la kushangaza" na kusema hakuna
mipango ya kumuuza mchezaji huyo (TalkSport).
Real Madrid wanafikiria kumchukua N'Golo Kante kutoka
Chelsea (Don Balon).
Manchester United hawajakata tamaa ya kumfuatilia mshambuliaji
wa Everton Romelu Lukaku, lakini watalazimika kulipa hadi pauni milioni 90
(Mirror).
Manchester United hawatoongeza dau lao la pauni milioni 26.4
ili kumsajili kiungo Ivan Perisic wa Inter Milan, na wana uhakika wa
kukamilisha mkataba huo (Calciomercato.com).
Liverpool huenda wakakamilisha usajili wa Mohamed Salah siku
ya Jumatano - leo- (Sky Sports).
Usajili mpya wa Liverpool Mohamed Salah anataka kuvaa jezi
namba tisa (Liverpool Echo).
Swansea watamsajili mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham,
19, kwa mkopo wa mwaka mmoja (Daily Mirror).
Swansea pia wamemuulizia beki wa zamani wa Liverpool Martin
Skirtel, 32, anayechezea Fernabahce (Daily Mail)
Wakala wa Zlatan Ibrahimovic Mino Raiola amesema mchezaji
huyo ameitwa na timu nyingi kutoka Marekani na kwingineko (Gazzetta dello
Sport).
West Ham wameanza mazungumzo ya mkataba mpya wa kiungo wao
Pedro Obiang, 25, ili kuzuia Everton, Sevilla na AC Milan zinazomfuatilia
(Daily Mirror).
Chelsea na Atletico Madrid wameanza mazungumzo kuhusu
mkataba wa pauni milioni 50 wa usajili wa Diego Costa. Ingawa Atletico wamefungiwa,
watamrejesha Costa kwa mkopo hadi Januari adhabu yao itakapomalizika (Mirror).
Chelsea wanamfuatilia winga wa Leicester City Riyad Mahrez,
wakati Conte akitaka kuimarisha safu ya ushambuliaji (Evening Standard).
Chelsea wanapanga kumtoa kwa mkopo Kurt Zouma msimu
unaokuja, wakati wakijiandaa kumsajili Leonardo Bonucci, 30 kutoka Juventus na
Virgil van Dijk, 25, kutoka Southampton (Evening Standard).
Chelsea wamekubaliana mkataba wa mshahara wa pauni 150,000
kwa wiki kumrejesha Romelu Lukaku Darajani kutoka Everton (Daily Star).
Chelsea wanakaribia kumsajili winga wa Middlesbrough Adama
Traore, 21 (Daily Star).
West Brom wanajiandaa kumpa mshahara wa pauni 100,000 beki
wao Jonny Evans, 29, na kumfanya mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya
klabu hiyo (Sun).
West Brom wametoa dau la pauni milioni 12 kumtaka
mshambuliaji wa Southampton Jay Rodriguez, 27, ingawa Burnley na Newcastle pia
zinamtaka (Daily Mail).
Beki wa Real Madrid, Pepe, 34, anasema hajaamua kuhusu
mustakbali wake, licha ya kuhusishwa na kuhamia PSG (ESPN FC).
Inter Milan wamemuulizia kiungo wa Barcelona Andres Iniesta
ambaye mkataba wake unamalizika mwakani (Gazzetta).
Beki wa Manchester City, Eliaquim Mangala, 26, yupo kwenye
mazungumzo ya kuhamia Lyon (Daily Mail).
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema mshambuliaji Olivier
Giroud, 30, bado ni mchezaji muhimu katika kikosi chake (Evening Standard).
Winga wa Watford Nordin Amrabat, 30, amehusishwa na kuhamia
Deportivio la Coruna (Watford Observer).
No comments