Shirika moja la ndege la
kibinafsi nchini India limemtuku safari za bure mtoto aliyezaliwa ndani ya moja
ya ndege zake, iliyokuwa safarini kutoka Saudi Arabia kuelekea nchini India.
Mhudumu mmoja wa ndege, ambaye alikuwa amepata
mafunzo ya uuguzi alimsaidia mama kujifungua mtoto umbali ya futi 35,000
angani.
Mama na mtoto wake walipelekwa hospitalini baada ya
ndege ya Boeng 737 kutua katika mji wa magharibi wa Mumbai.
Shirika hilo lilitoa taarifa kwenye kituo cha habari cha BBC kutoka Uingereza kuwa mama na mtoto wake
walikuwa katika afya nzuri.
Kampuni iliwashukuru wahudumu kwa kumsadia mama
kujifungua salama.
Shirika hilo lililisema kuwa ndiyo mara ya kwanza
mtoto kuzaliwa kwenye ndege yake.
Lakini mashirika kadhaa yamekumbanana hali kama
hiyo. Wahudumua wa shirika la ndege la uturuki wallisherehekea kuzaliwa kwa
mtoto msichana ndani ya ndege mwezi Aprili mwaka huu.
No comments