Header Ads

Baby Madaha - Mimi si shabiki wa Vanessa Mdee hata muziki wake

Msanii wa muziki ambaye ni zao la shindano la kusaka vipaji BSS, Baby Madaha amedai kuwa Vanessa Mdee si msanii mkali kama baadhi ya watu wanavyosema.
Muimbaji huyo amesema kwamba yeye anaamini kuna wasanii wakali zaidi yake lakini hawapewi nafasi wanayostahili kama anayopewa muimbaji huyo anayechanja mbuga zaidi kimataifa.
“Mimi si shabiki wa Vanessa hata muziki wake, hata nyimbo zake sizisikilizi kabasa,” alisema Baby Madaha. “Kuna wasanii wakali hawapewi tu nafasi, mimi ni shabiki wa Lady Jaydee, akina Mwasiti kuna wasanii wengi wanafanya muziki nzuri,”
Madaha amedai hamuonei wivu Vanessa Mdee kutokana na mashavu anayopata ila kuna baadhi ya sifa anapata ambazo sio saizi yake.
Muimbaji huyo anajipanga kuachia wimbo mpya hivi karibuni baada ya kuwa amekaa muda mrefu bila kuachia wimbo mpya.

No comments

Powered by Blogger.